Msanii wa mziki wa Injili Martha baraka kutoka Tanzania amezindua albamu yake ya pili kwa jina Furaha.
Akizungumza na Dominick Mwambui kwenye kipindi Simama Tushangilie asubuhi ya leo, Martha amefichua kuwa albamu hiyo inazungumzia sana mapito aliyoyapitia.
Kulingana naye alipitia kipindi kigumu maishani mwake lakini mambo yalibadilika punde Mungu alipomuinua.
“Haikuwa maamuzi yangu binafsi kufanya mziki wa Injili bali kulikuwa na msukumo wa Kimungu ndani yake ndipo nikajipata nafanya mziki huu…Najua kuna watu hupitia vipindi vigumu lakoni albamu hii kwa sana inazungumzia historia yangu na jinsi Mungu alivyonipa Furaha,” amesema Martha.
Hapo awali msanii huyu aliwahi kuvuma na kibao jina la Yesu ni dawa.
Unaweza kutizama kazi zake hapa.
Taarifa na Radio Kaya.