Marwa awasihi Wapwani kudumisha Amani ili kuimarisha utalii

December 4, 2017

Mshirikishi Mkuu wa Utawala kanda ya Pwani Nelson Marwa amewasihi waakazi wa Pwani kuzidi kudumisha amani ili sekta ya utalii iimarike.

Akiongea na wanahabari mjini Mombasa Marwa amesema kuwa tayari sekta ya utalii imeanza kuimarika kwani watalii kutoka mataifa mbali mbali wamenza kuwasili kwa wingi.

Marwa aidha amefichua kwamba tayari hoteli mbali mbali zimeanza kuwaajiri wafanyikazi waliokuwa wameachishwa kazi baada ya sekta ya utalii kudorora hali ambayo ameitakja kuwa itaimarisha uchumi.

Taarifa na Hussein Mdune.

[Nyumba yangu haina mlango]

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.