MASHINE ZA KAMARI ZAHARIBIWA LIKONI

June 14, 2018

Idara ya usalama katika eneo la Likoni imechoma zaidi ya mashini 42 za kuchezea kamari katika eneo hilo.

Akiongea katika shughuli ya uchomaji mashine hizo, kaimu kamishna gatuzi dogo la Likoni Bi. Jane Macharia amesema hatua hiyo ni njia moja wapo ya kukabiliana na visa vya wizi miongoni mwa vijana wa eneo hilo.

Akiwatahadharisha wafanyibiashara, Bi. Macharia amesema idara ya usalama eneo hilo haitaruhusu biashara ya kamari na atakayepatikana atachukuliwa hatua za kisheria.

Taarifa na Hussein Mdune

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.