Mashini 30 za mchezo wa Kamari kuharibiwa Kwale

June 25, 2018

Idara ya usalama kaunti ya Kwale inapanga mikakati ya kuharibu mashine 30 za mchezo wa kamari zilizonaswa kufuatia msako unaondelea katika kaunti hiyo kama njia moja wapo ya kuangamiza mchezo huo.

Kamishna wa kaunti ya Kwale Karuku Ngumo amesema tayari ametoa amri kwa maafisa wa polisi pamoja na machifu kuendeleza msako wa mashine hizo ili kuhakikisha jamii haipotoshwi kimaadili.

Ngumo amedai kuwa amepokea ripoti kutoka kwa baadhi ya wanajamii kuwa wazazi hususan wa kike wametelekeza familia zao kwa kutumia fedha za matumizi katika michezo ya kamari na kuchangia watoto kukosa masomo.

Wakati uo huo ameitaka jamii kushirikiana na idara ya usalama kuhakikisha kuwa mchezo wa kamari unazikwa katika kaburi la sahau.

Taarifa na Mariam Gao.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.