Matapeli waokolewa na Polisi baada ya kushambuliwa na wananchi Kwale

November 6, 2018

Watu wawili wanaoshukiwa kuwa matapeli wamepokea kichapo cha mbwa kutoka kwa wananchi baada ya kushikwa kwenye harakati ya kutekeleza wizi wa Pesa.

Wawili hao wanaotoka katika kaunti ya Kisii, wamejipata kwenye mikono ya wananchi waliojawa ghadhabu, baada ya kumwibia Selina Dima, mfanyibiashara wa nguo mjini Kwale shilingi elfu 11 kutoka kwa simu yake.

Kulingana na mama huyo, washukiwa hao walijaribu kutoroka baada ya kuiba pesa hizo lakini wakamatwa mda mfupi baadaye kupitia ushirikiano wa wananchi.

Akithibitisha kisa hicho, Afisa wa Polisi anayesimamia kituo cha polisi cha Kwale Ludwin Sasati, amesema washukiwa hao ni miongoni mwa wahalifu wanaowalaghai wananchi, huku akieleza kuwa watafikishwa mahakamani hapo kesho.

Sasati hata hivyo amewatahadharisha wananchi dhidi ya mapateli wanaotumia mbinu mbalimbali kuwaibia pesa zao.

Taarifa na Michael Otieno.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.