Matiangi ahimizwa kukabiliana na mihadarati Pwani

February 5, 2019

Kiongozi wa vijana katika Kaunti ya Mombasa Bi Mirajj Abdallah amemtaka Waziri wa usalama wa ndani Dakta Fred Matiang’i kulishughulikia kikamilifu tatizo la dawa za kulevya katika Ukanda wa Pwani.

Mirajj amesema kwamba swala hilo limekuwa tata na kupelekea kudidimia kwa usalama katika maeneo mengi ya ukanda wa Pwani.

Akizungumza Mombasa, Mirajj amesema kwamba ni sharti swala la dawa za kulevya lichukuliwe kwa uzito kukabili utumizi wa mihadarati na biashara yao haramu.

wakati uo huo amemtaka Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Evans Achoki kutowasaza walanguzi wa dawa za kulevya akisema kwamba walanguzi hao wanazidi kukiangamiza kizazi kichanga cha Kaunti hiyo.

Hata hivyo, kwa mara nyingine tena Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Evans Achoki amewarai Wakaazi wa Kaunti hiyo kuwafichua walanguzi wa mihadarati akisema kwamba japo wanawajua vyema wamesalia kimya.

Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.