Mbunge aliyekuwa mgema

January 8, 2018

Maisha ni panda shuka na haijalishi pale unapoanzia kwani una uwezo wa kuwa chochote maishani.

Huu ndio ujumbe uliotolea na Mbunge wa sasa wa Ganze Teddy Mwambire baada ya kufichua kuwa aliwahi kupitia kipindi kigumu maishani kabla mambo yake hayajamnyokea.

Mbunge huyo amefichua kuwa aliwahi kuwa mgema wa pombe ya mnazi wakati mmoja maishani ili aweze kugharamia karo yake ya shule.

Kupitia kwa kipande cha video alichokipachika kwenye mtandao wa kijamii Mbunge huyo aliudhihirishia ulimwengu kuwa ni mgema stadi kwa kukwea mnazi ulioko katika shamba lao la  Forodhoyo na kuangua nazi.

Mtizame hapa.

 

Kando na kuwa mgema Mbunge huyo aliongezea kuwa aliwahi kuwa mfanyikazi wa shamba mjini Malindi kabla ya kuajiriwa kama muuzaji maji tamu.

Taarifa na Dominick Mwambu.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.