Mbunge ataka biashara ya madafu iimarishwe

February 10, 2019

TANDAZA

Mbunge wa Matuga Kassim Sawa Tandaza amewataka viongozi wa kisiasa hapa Pwani kushirikiana na kutafuta mbinu za kuimarisha biashara ya madafu.

Akihutubia viongozi wa muungano wa wafanyibiashara wa madafu Tandaza amesema wafanyibiashara wa madafu wanapitia changamoto nyingi na kuna haja ya kuwatafutia soko katika mataifa ya nje ili wajiimarishe kimaisha.

Hata hivyo amewataka wafanyibiashara kuuza madafu yao kwa bei maalum,akisema kuwa zao hilo linavutia wengi ikiwemo watalii.

Kwa upande wake mwenyekiti wa muungano wa wafanyibiashara wa madafu Hamis Rashid Mwajita amekashifu hatua ya baadhi ya wafanyibiashara wa madafu wanaouza bidhaa hio kwa bei ya chini.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.