Mbunge awaonya wanafunzi dhidi ya kushiriki ngono kiholela

May 1, 2018

Mbunge wa Jomvu Badi Twalib amewaonya wanafunzi wa eneo bunge lake dhidi ya kujihusisha na ngono za kiholela wakiwa katika umri mdogo na badala yake akawata wazingatie zaidi elimu yao.

Akizungumza katika eneo bunge la Jomvu, Badi amesema mara nyingi wanafunzi hupotoka kimaadili kutokana na kutoshirikishwa katika mijadala au kupewa mwelekeo unaostahili kutoka kwa wazazi wao.

Ameongeza kuwa baadhi ya viongozi wa kijamii wanastahili kuwahimiza wanafunzi hasa wale wa shule za msingi na upili kuzingatia elimu.

Wakati uo huo amedai kuwa wanafunzi kutoka familia zisizojiweza watapata ufadhili wa masomo kupitia hazina ya CDF ili wakamilishe masomo yao, huku akisema tayari wanafunzi 2,650 wamenufaika na kima cha shilingi milioni 13 kutoka hazina hiyo.

Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.