Mbunge kutumia pesa za CDF kujenga shule ya kitaifa

June 8, 2018

OWEN NA KINGI

Mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya amesema kwamba atatumia pesa za ustawi wa eneo bunge (CDF) ili kujenga shule ya kitaifa katika eneo bunge lake.


Akizungumza wakati wa hafla ya kutuzwa kwa wanafunzi waliofanya vyema katika eneo bunge lake Owen amesema kuwa atatumia mgao wa pesa wa mwaka wake wa tatu mamlakani kujenga shule hiyo itakayogharimu  kima cha milioni 130.

Kwa upande wake Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Jefwa Kingi amewataka wakaazi wa Kilifi kujiepusha na kasumba kuwa wakaazi wa Kilifi hawasomi.

Aidha ameipa changamoto jamii ya wapwani kujiuliza ni kwa nini viwango vya elimu viko chini.
Kingi amewataka walimu, wazazi na serikali kushirikiana vilivyo ili kuitatua changamoto ya elimu.

Kingi aidha ameikosoa serikali kuu kuhusu ugavi wa walimu na miundo msingi. Kulingana na Gavana huyo kaunti za Pwani hupawa walimu wachache na mgao mdogo wa kuendeleza miundo misingi.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.