Mbunge wa Changamwe aunga mkono msako wa Polisi

June 7, 2018

mwinyi1

Huku Idara ya Usalama katika Kaunti ya Mombasa ikiendeleza msako kuwakamata vijana waliojiunga na magenge ya uhalifu yanayotatiza usalama katika baadhi ya maeneo ya kaunti hiyo, Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi amewahimiza wazazi kuwajibikia  majukumu yao ya ulezi.

Mwinyi amesema kwamba kuzembea kwa baadhi ya wazazi katika majukumu yao ya ulezi ndio chanzo kikuu Cha vijana kupotoka kimaadili na  kujihusisha na vitendo vinavyoathiri usalama.

Akizungumza huko Changamwe Mwinyi ameeleza imani yake kwamba wazazi wakiwajibikia kikamilifu majukumu yao ya ulezi, visa vya utovu wa usalama vitakomeshwa.

Kauli ya Mwinyi inajiri huku Vijana 20 zaidi wanaoshukiwa kuwa wanachama wa magenge ya kihalifu wakitiwa  nguvuni na maafisa wa polisi katika eneo la kisauni usiku wa kuamkia leo na kufikisha 160 idadi ya vijana waliokamatwa na polisi kufuatia msako unaoendelezwa   eneo hilo la Kisauni .

Taarifa na Cyrus Ngonyo.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.