Mbunge wa Kinango asisitiza kuwa NASA walenga kuleta maendeleo

January 13, 2018

Mbunge wa Kinango  Benjamin Tayari amepinga vikali madai  ya  viongozi wa  chama cha Jubilee kaunti ya  Kwale, kuwa  viongozi wa Muungano wa NASA katika  kaunti hiyo wanalenga kusambaratisha juhudi za maendeleo za Gavana Salim Mvurya .

Tayari amesema kuwa hana nia ya kusambaratisha juhudi za maendeleo ya Serikali ya kaunti ya Kwale, akiyataja madai hayo kama yasiokuwa na msingi  wowote na yanalenga kuwaharibia sifa viongozi wa upinzani.

Akigusia suala la bunge la Wananchi, Mbunge huyo wa Kinango amewakashfu baadhi ya viongozi wa chama cha Jubilee kwa kumsuta mjumbe wa Wadi ya Mwavumbo Joseph Ndeme aliyewasilisha bungeni mswada wa kuunda kwa bunge la wananchi na kupitishwa.

Amedokeza kuwa katiba inaruhusu wananchi kutengeneza bunge na kutoa maoni yao kuhusiana na masuala mbalimbali yanayoenda kinyume na matarajio yao.

Taarifa Michael Otieno.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.