Mbunge wa Likoni aitaka serikali kuongeza juhudi za kukabiliana na Mihadarati

January 10, 2018

Mbunge wa Likoni Bi Mish Mboko ameitaka serikali kuongeza juhudi zake za kuwakabili walanguzi wakuu wa mihadharati  katika Ukanda wa Pwani.

Akizungumza mjini Mombasa, Bi Mboko amehoji kuwa ni jukumu la serikali kukabiliana na walanguzi hao sawia na kueka sheria kali zitakazowazuia kufanya biashara hiyo.

Bi Mboko amesema kuwa idara ya Mahakama nayo inafaa kuwaadhibu washukiwa wakuu wanaokabiliwa na kashfa hizo huku akivilaumu vitengo vya usalama kwa kutowakabili vikali wahushika wakuu.

Mbunge huyo wa Likoni hata hivyo amesema kuwa swala la mihadarati katika ukanda wa Pwani limekuwa sugu na hata kusababisha madhara makubwa kwa vijana wenye umri mdogo.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.