Mbunge wa Likoni awalaumu polisi kwa kushindwa kuwakabili walaguzi wa mihadarati

November 23, 2017

Mbunge wa Likoni Bi Mishi Mboko ameilaumu idara ya usalama kwa kushindwa kukabiliana na walanguzi wakuu wa mihadarati katika eneo la Likoni.

Bi Mboko anasema kuwa licha ya maafisa wa polisi kuwatambua wanaojihusisha na biashara hiyo haramu hakuna hatua zozote za kisheria zimechukuliwa dhidi ya wahusika wakuu wa mihadarati.

 Akizungumza na Wanahabari baada ya Kongamano la kujadili masuala ya afya lililoandaliwa na Shirika la Msalaba Mwekundu mjini Mombasa, Bi Mboko amewailaumu polisi kwa kuonyesha utepetevu kwenye swala hilo.

Mbunge huyo wa Likoni amefichua kuwa zaidi ya watu 650 wanatumia mihadarati katika eneo la Likoni na akaitaka serikali kuidhinisha mpango wa kujenga vituo maalumu vya kuwarekebisha tabia watumizi hao.

Taarifa na Cyrus Ngonyo.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.