Mbunge wa Magarini kuwasilisha hoja bungeni kuhusu kampuni ya chumvi

July 2, 2018

Mbunge wa Magarini kaunti ya Kilifi Michael Kingi anapania kuwasilisha hoja bungeni kuhusiana na ripoti iliyotolewa na Tume ya  kutetea haki za kibinadamu la Kenya National Commission on Human Rights majuma matatu yaliyopita, kuhusu utenda kazi wa kampuni za chumvi kwa wakazi wa eneo hilo.


Hatua hii inajiri baada ya baadhi ya viongozi kutoka kaunti ya Kilifi wametofautiana vikali na ripoti hiyo wakidai kuwa haikuwa na ukweli wowote na badala yake ilikuwa inanyanyasa na kuwakandamiza wananchi.

Kingi amedokeza kuwa hatua yake ya kuwasilisha hoja hiyo bungeni itahakikisha kamati zinazoangazia haki za kibinadamu bungeni zinachunguza kwa kina ripoti hiyo.

Endapo itapatikana na makosa bunge litawachukulia hatua kali za kisheria wahusika.

Taarifa na Esther Mwagandi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.