Mbunge wa Mwatate aagiza uchunguzi kufanywa kuhusu uingizwaji wa bidhaa ghushi

June 29, 2018

Mbunge wa eneo bunge la Mwatate kaunti ya Taita Taveta Andrew Mwadime, sasa anataka kuchunguzwa kwa kina, maafisa wanaohusika na uingizwaji wa bidhaa mbali mbali nchini ikiwemo vyakula na kukabiliana vikali na wanaoingiza bidhaa ghushi zisizofaa kwa matumizi ya binadamu.

Mwadime amesema kuwa ufisadi miongoni mwa maafisa hao waliotwikwa jukumu kuangalia ubora wa bidhaa zinazoingizwa nchini, umepelekea uingizaji wa bidhaa zisizofaa kwa matumizi wa binadamu ikiwemo sukari inayodaiwa kuwa na madini ya chuma na zebaki.

Mwadime amesema kuwa utumizi wa bidhaa hizo umechangia ongezeko la magonjwa mbali mbali ikiwemo saratani.

Kiongozi huyo anaunga mkono mwito wa rais Uhuru Kenyatta wa kuchunguzwa kwa maafisa mbali mbali nchini kubaini walivyopata mali zao, akisema italiokoa taifa hili na wafisadi.

Taarifa na Fatuma Rashid.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.