Mbunge wa Rabai amtaka Naibu rais kuacha kuwapotosha wakenya

June 25, 2018

KINGI JUMWA KAMOTI

Wakaazi wa Pwani wameshauriwa kupuuzilia mbali mienendo ya baadhi ya viongozi wa kisiasa humu nchini wanajipendekeza kuungwa mkono kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.


Mbunge wa Rabai William Kamoti amesema kuna haja ya wananchi kusahau maswala ya kisiasa kwa sasa na kuunga mkono mikakati ya Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa NASA Raila Odinga inayolenga kuwanufaisha kimaendeleo.

Akizungumza kwenye mazishi ya Mwalimu katika wadi ya Ruruma kaunti ya Kilifi, Kamoti amemtaka Naibu Rais William Ruto kusitisha kuwapotosha wananchi kwa azma yake ya kuwania urais mwaka wa 2022, akisema ni mapema mno kufanya siasa.

Kwa upande wake Mwakilishi wa wadi ya Ruruma kaunti ya Kilifi,Jana Tsuma Jana amewahakikishia walimu wa shule za chekechea kuwa wadi yake itawadhamini walimu 50 kujiunga na mafunzo ya uwalimu.

Taarifa na Mercy Tumaini.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.