Mbwana kuelekea Mahakama ya rufaa kupinga ushindi wa Mvurya

November 16, 2017

Jopo la Mawakili wanaomwakilisha mlalamishi Mwamlole Tchappu Mbwana aliyepinga ushindi wa Salim Mvurya, sasa linaelekea katika mahakama ya rufaa baada ya mahakama kuu Mjini Mombasa kutupilia mbali kesi hiyo.

Jopo hilo likiongozwa na wakili Tom Ambwere, Anthony Wasuna na Bi Cheri Oyier limesema kwamba halikubaliani na uamuzi wa Jaji Mugure Thande wa kutupilia mbali kesi hiyo.

Mawakili hao sasa wameomba kukabidhiwa stakabadhi za kesi hiyo na uamuzi huo wa mahakama katika muda wa siku nne zijazo ili kuwasilisha kesi hiyo katika mahakama ya rufaa kabla ya muda wa siku 14 kukamilika.

Jaji Mugure Thande amemuamuru mlalamishi Mwamlole Tchapu Mbwana kulipa kima cha shilingi milioni 2.5 kama gharama ya kesi.

Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.