Mchanganyiko wa dini na siasa wasababisha uongozi duni Pwani

July 3, 2018

Hatua ya viongozi wa kidini kujiunga na mirengo ya kisiasa imetajwa kuchangia muongozo duni kwa jamii ya ukanda wa Pwani.

Akiongea kwenye mdahalo wa kujadili maswala ya kiusalama na Amani mjini mombasa , afisa mkuu mtendaji wa baraza la viongozi wa kidini Pwani Coast Interfaith Council Of Clerics  Steven Anyenda amesema ni jambo la kushangaza  kuona viongozi wa kidini wakipigia upato maswala ya vyama vya kisiasa.

Anyenda amewataka viongozi hao kukomesha tabia hio akisema kuwa viongozi wa kidini hawapaswi kuweka wazi misimamo yao ya ksiasa ikizingatiwa kwamba wanaongoza waumini wanaoegemea mirengo mbali mbali.

Hata hivyo amesema kuwa ni jukumu la viongozi wa kidini kushirikiana vyema na viongozi wa kisiasa pasi kuzingatia kigezo cha mrengo wa kisiasa kwa manufaa ya waumini wao.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.