Mdudu anayeguguna tasnia ya burudani Pwani ajulikana

November 24, 2017

Kwa siku nyingi watu wamekuwa wakijadiliana kuhusu mdudu anayeguguna tasnia ya burudani ukanda wa Pwani.

Tatizo hili lilipelekea washikadu mbalimbali kuandaa mikutano ili kubaini kwa undani swala hili. Hata hivyo kulingana na msanii Peter Siku maarufu kama Pday ukosefu wa pesa ndio mdudu anayeguguna tasnia ya burudani.

Pday ambaye hivi majuzi ameachilia kibao Subira pamoja na bendi ya Mtawali’s anashikilia kuwa wadau wengi hukimbilia pesa badala ya ubora wa  kazi.

Aidha amesema kuwa endapo watu watazingatia ubora wa kazi badala ya ulafi wa pesa basi tasnia ya muziki ya hapa Pwani itaweza kukua na kuwa na faida kwa wasanii.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.