Meli ya watalii elfu yawasili Mombasa

January 4, 2018

Sekta ya utalii humu nchini imezidi kupigwa jeki baada ya meli yenye watalii elfu moja kutia nanga katika bandari ya Mombasa.

Meli hiyo kwa jina MS Nautica ilikuwa imebeba watalii kutoka mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini.

Akizungumza baada ya kupokea meli hiyo afisa wa uhusiano mwema katika bandari ya Mombasa Hajji Masemo amesema kuwa watalii hao watazuru vivutio mbali mbali vya watalii Pwani.

Masemo aidha amedokeza kwamba Meli tatu zaidi zinatarajiwa kuwasili kwenye bandari hiyo ya Mombasa kabla msimu wa watalii kukamilika mwezi Machi mwaka huu.

Taarifa na Cyrus Ngonyo.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.