Mfumo wa kusajili wanafunzi kidigitali wakosa kutumika Kwale

January 9, 2019

Mwalimu mkuu wa shule ya upili yaGolini, Changawa Shungu.

Mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Golini, Changawa Shungu.

Huku mfumo mpya wa kidijitali wa kuwasajili wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza ukiendelezwa nchini, shule za mashinani zimeripotiwa kukabiliwa na changamoto za mtandao kufanikisha mfumo huo.

Katika shule ya upili ya Golini, kaunti ya Kwale, Naibu mwalimu mkuu wa shule hiyo Changawa Shungu Madaraka, amesema kuwa   jumla ya wanafunzi 15 waliojiunga na kidato cha kwanza   katika shule hiyo, wamesajiliwa kupitia mfumo wa  zamani,  na  majina yao yatatumwa  kwa wizara ya elimu kupitia mfumo huo mpya baadae.

Hata hivyo ameupongeza mfumo huo mpya, akisema kuwa utaziwezesha shule za viwango vya chini kupata idadi kamili ya wanafunzi waliotengewa nafasi katika shule hizo na kuchangia ushundani wa kimasomo.

Haya yanajiri huku   wizara ya elimu ikiagiza usajili wa wanafunzi kupitia mfumo huo mpya kukamilika tarehe 11 mwezi huu wa Januari.

Taarifa na Michael   Otieno.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.