Mgawanyiko wa kisiasa ndio chanzo cha kudorora kwa maendeleo Pwani

January 13, 2019

22 06 18 - NUREIN MWATSAHU.

Mchanganuzi wa masuala ya kisiasa kaunti ya Mombasa Ali Mwatshu amesema kuwa mgawanyiko miongoni mwa viongozi wa kisiasa humu nchini umechangia taifa hili kubaki nyuma kimaendeleo.

Mwatsahu amesema viongozi wanapaswa kujiotenga na migogoro ya mara kwa mara miongoni mwao badala yake kuangazia mbinu za kuimarisha uchumi wa taifa.

Wakati uo huo amewataka viongozi wa kisiasa kukoma kuzungumzia ushirikiano kati ya rais uhuru kenyatta na kinara wa odm raila odinga.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.