MIAKA 15 GEREZANI KWA KUMDHULUMU MWANAFUNZI

November 30, 2018

Mahakama ya Malindi imemhukumu kifungo cha miaka 10 gerezani mwanamume mmoja baada ya kumpata na hatia ya kushiriki ngono na mtoto mwenye umri wa miaka 15.

Inadaiwa kuwa mwanamume huyo kwa jina Onesmus Safari ambae ni mwalimu wa mchezo wa Taekwondo, alishiriki ngono na msichana huyo ambae alikua mwanafunzi wake tarehe 20 mwezi novemba mwaka 2015 wakati wa mashindano ya mchezo huo eneo la Watamu.

Hakimu mkuu mwandamizi wa mahakama hio Silvia Wewa amesema kuwa uamuzi huo haukujumuisha  kosa la pili la unajisi ambapo mshatakiwa angetumikia  kifungo cha miaka 15 gerezani akiwa na hatia.

Hata hivyo mshtakiwa amepewa muda wa siku 14 kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama.

Taarifa na Charo Banda

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.