Milioni 20 zatengewa elimu Malindi

June 23, 2018

Sekta ya elimu huko Malindi kaunti ya Kilifi imepigwa jeki zaidi baada ya afisi ya eneo bunge hilo kutenga jumla ya shilingi milioni 20 kwa ujenzi wa afisi za elimu.

Akiongea baada ya kuweka jiwe la msingi, Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa amesema chini ya uongozi wake atatumia kila raslimali alizotengewa na serikali kuhakikisha viwango vya elimu vinaboreshwa katika eneo hilo.

Jumwa ambaye alikuwa ameandamana na wadau mbalimbali wa elimu akiwemo Afisa mkuu wa elimu kaunti ndogo ya Malindi Veronica Kalungu amehoji kuwa ukosefu wa mazingira bora ya wanafunzi na walimu ndio changamoto kuu.

Wakati uo huo amepinga vikali hatua ya walimu wakuu kuhamishwa hadi shule zengine, akisema hatua hiyo imechangia walimu kukosa motisha ya kufundisha shuleni.

Taarifa na Charo Banda.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.