Mipango ya Diamond mwaka 2019

January 6, 2019

DIAMOND

Baada ya kufunga mwaka wa 2018 na mafanikio makubwa katika biashara ya mziki, msanii Diamond Platnumz kutoka nchini Tanzania ameelezea nia yake ya kuendelea kugandamiza kimziki mwaka wa 2019.


Diamond amefichua mipango yake ya mwaka 2019 kwa mashabiki.

Diamond anasema mwaka wa 2109 analenga kusukuma brand yake zaidi ili ivuke mipaka ya Afrika Mashariki hadi katika soko la kimataifa.

Aidha Diamond angependa kufanya collabo na wasanii zaidi wa kimataifa, huku akilenga zaidi kusukuma lugha ya Kiswahili mbele ya jamii ya kimatifa kupitia nyimbo zake katika sehemu tofauti za dunia.

Kufikia sasa Diamond amefanya collabo na wasanii tofauti wa kimataifa ikiwemo Omarion, Rick Ross, Neyo na Morgan Heritage.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.