Mjumbe wa Wadi ya Kinondo aapishwa

May 11, 2018

Omar Hamis maarufu Pweza, ameapishwa rasmi kuhudumu kama Mjumbe wa Wadi ya Kinondo katika kipindi cha miaka 5 ijayo.

Hafla ya kuapishwa kwake imeongozwa na Spika wa bunge la kaunti ya Kwale Sammy Ruwa, kwenye kikao maalum cha bunge hilo mapema leo.

Akiongea na Wanahabari baada ya kuapishwa kwake, Pweza amewapongeza wakaazi wa Wadi ya Kinondo kwa kuwa na imani naye, huku akiahidi kuwatumikia kwa kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo.

Aidha amewasihi wapinzani wake waliowania kiti hicho kuunga mkono uongozi wake kwa ajili ya kuboresha maisha ya wakaazi wa Kinondo.

Taarifa na Michael Otieno.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.