Mkufunzi wa Assad alalamikia makali ya mfungo

May 28, 2018

Mkufunzi wa klabu ya SS Assad Ben Tole amesema kwamba ukosefu wa mashabiki  sawia na saumu ya mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani miongoni mwa wachezaji wake huenda kwa kiasi fulani ulichangia wao kupoteza mechi ya Ngao ya Sportpesa dhidi yao na mabingwa wa ligi kuu nchini KPL Gor Mahia.


Tole amekisifia kikosi chake kwani kilionyesha umahiri mkubwa katika dakika 20 za kwanza.

Aidha ameishinikiza serikali ya kaunti ya kwale kuufanyia ukarabati uwanja wa maonyeshoya kilimo wa ukunda ili mechi zijazo zichezwe katika uwanja wao wa nyumbani.

Ss Assad ilikubali kipigo cha magoli 5-1 kutoka kwa Gor Mahia ,wafungaji wa Gor walikuwa ni Lawrence Juma aliyetia kimiani mabao mawili, Godfrey Walusimbi, Eluid Lokuwam na Jaques Tuyisenge waliofunga bao moja kila mmoja.

Upande wa Gor Mahia mkufunzi Dylan Kerr ameisifia klabu ya Assad na kuwapa moyo wa kuzidi kufanya vyema kimchezo.

Taarifa na Cyrus Ngonyo.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.