Mkufunzi wa Bandari alalamikia majeruhi

May 6, 2018

Mkufunzi wa Bandari ken odhiambo amesema kwamba majeruhi kwenye kikosi chake sawia na hali duni ya uwanja ilichangia kwa kiasi kikubwa timu yake  kupoteza mechi kati yao na Tusker katika uwanja wao nyumbani wikendi iliyopita.

Odhiambo amesema kwamba wachezaji muhimu wa kiungo cha kati walijeruhiwa kwenye mechi dhidi yao  na Nakumatt hivyo kuathiri kiungo cha kati cha timu hiyo.

Amelitaka shirikisho la soka nchini FKF kuidhinisha sheria zitakazo walinda wachezaji na kuhakikisha mchezaji yoyote atakaye cheza vibaya anapewa adhabu ya kutoshiriki  mechi kadhaa.

Bandari ilipokea kipigo cha 2-0 dhidi ya Tusker  wikendi iliyopita kikiwa kipigo cha kwanza nyumbani msimu huu.

Taarifa na Cyrus Ngonyo.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.