Mlolwa apendekeza kujengwa kwa masoko ya mifugo Voi

June 7, 2018

Mbunge wa Voi Jonnes Mlolwa ameeleza umuhimu wa kuwepo kwa  masoko ya mifugo katika kaunti hiyo.

Mlolwa amesema kupitia masoko hayo mwanachi atauza mifugo wake kwa bei nzuri na kuwezeshwa kukidhi mahitaji yake mbalimbali.

Mlolwa ameitaka wizara husika kuhakikisha kuwa hilo linafanyika ili kumuwezesha mfugaji kupata faida nzuri kutokana na shughuli zake za ufugaji.

Taarifa na Fatuma Rashid.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.