Mmiliki wa gorofa iliyoanguka Malindi akamatwa

October 30, 2018

Maafisa wa kitengo cha upelelezi wa jinai eneo la Malindi wamemtia nguvuni  mmiliki wa jumba la ghorofa nane lililoporomoka mjini humo siku chache zilizopita na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine  23 wakipata majeraha mabaya.

Akiongea na wanahabari afisini mwake afisa mkuu wa upelelezi wa jinai eneo hilo Antony Sunguti amesema tayari wameanza kumhoji jamaa huyo kwa jina Shabir Ali Fakhurddin kuhusiana na mkasa huo.

Kulingana na Sunguti Jamaa huyo alikuwa amejificha katika kaunti ya Mombasa kabla ya kujisalimisha katika kituo cha polisi cha Malindi na hatimaye akatiwa mbaroni.

Sunguti ameongeza kuwa idara hio inawasaka maafisa zaidi wakiwemo wale wa serikali ambao walihusika na ujenzi wa jumba hilo.

Taarifa Charo Banda.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.