Modern Coast Rangers yasaka mkufunzi

January 1, 2018

Klabu ya Modern Coast Rangers inatafuta mkufunzi mpya baada ya aliyekuwa mkufunzi mkuu wa klabu hiyo, Ahmed Mohamed maarufu kama Moha kuhamia klabu ya Wazito FC.

Kulingana na katibu wa klabu hiyo Ferdinand Ogot klabu hiyo ipo katika mazungumzo na wakufunzi kadhaa walio onyesha nia ya kuchukua mikoba ya klabu hiyo.

Mkufunzi mpya wa klabu hiyo atatwikwa jukumu la kuchagua wachezaji wapya katika majaribio yatakayo anza tarehe 8 Januari.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.