Modern Coast Rangers yatema wachezaji saba

December 21, 2017

Klabu ya Modern Coast Rangers  imeagana na wachezaji saba.

Miongoni mwa wachezaji hao ni mshambuliaji matata aliyewahi kuchezea Batoto Ba Mungu Benjamin Asuman.

Kulingana na katibu wa klabu hiyo Ferdinand Ogot uamuzi huo uliafikiwa baada ya majadiliano ya kina na usimamizi wa klabu hiyo.

Wengine waliotemwa ni Abdul Maina, Abdala Mdeka,Ibrahim Wanga, walinzi Naftali Orawo Amayo, Hamisi Mwachihande na Kevin Owino.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.