Moto wateketeza mkahawa wa BidiBadu, Ukunda

October 15, 2018

Mali ya thamani isiyojulikana imechomeka katika hoteli ya bidibadu baada ya moto kuteketeza mkahawa huo.

Akithibitisha tukio hilo afisa mkuu wa polisi eneo la msambweni joseph chebusit amesema kwamba moto huo umeshika kwenye paa la makuti ambapo kulikuwa na upepo mkali.

Chebusit amesema kwamba moto huo umeanzia jikoni lakini bado chanzo cha moto huo hakijajulikana.

Hata hivyo hakuna mtu aliyejeruhiwa na kwasasa uchunguzi umeanxishwa ili kubaini chanzo cha moto huo.

Taarifa na Salim Mwakazi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.