Mozenga kuzindua bendi yake rasmi wikendi

May 8, 2018

Mtayarishaji wa mziki wa Bango Moses Tsuma maarufu kama Mozenga analenga kuzindua rasmi bendi yake ya mziki wikendi hii mjini Kilifi.

Mozenga anayesifika kwa kuchanganya msingi wa sengenya na Bango anasema amechukua hatua hiyo baada ya kuhudumu katika bendi mbalimbali za mziki.

“Hakuna bendi ya mziki ambayo sijafanya kazi nayo. Nimeamua kuunda baendi yangu baada ya kusoma mengi nilipokuwa katika bendi hizi,”amesema Mozenga.

Bendi hiyo itafahamika kama Maridhia Sounds Band.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.