Mruttu atofautiana na viongozi wanaohimiza wananchi kuzaana kwa wingi

September 6, 2018

Aliyekuwa Gavana wa kaunti ya Taita Taveta John Mruttu ametofautiana na baadhi ya viongozi eneo hilo wanaowashauri wakaazi kuzaa kwa wingi ili kuongezeka idadi ya wakaazi eneo hilo.

Viongozi hao walitoa pendekezo hilo baada ya tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kutishia kuvunja baadhi ya maeneo bunge yenye idadi ndogo ya wakaazi.

Mruttu anasema kuzaa hasa wakati huu ambapo gharama ya maisha inazidi kupanda nchini sio suluhu bali viongozi wanapaswa kushinikiza mageuzi kwa sheria husika.

Mruttu amesema gharama ya juu ya maisha hairuhusu wanananchi kuzidi kuzaa watoto ambao watashindwa kukidhi mahitaji yao msingi.

Taarifa na Fatuma Rashid.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.