Msafirishaji makaa apigwa risasi Malindi

November 8, 2018

Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 27 katika eneo la Marafa huko Magarini kaunti ya Kilifi anauguza majeraha katika hospitali ya Malindi  baada  ya kudaiwa kupigwa risasi na polisi.

Jumaa Safari ambaye alikuwa akisafirisha magunia matatu ya makaa kutoka Marafa kuelekea Malindi anadaiwa kupigwa risasi alipokaidi amri ya maafisa waliokuwa wanashika doria ambao walimtaka kusimama.

Afisa mkuu wa polisi eneo la Magarini Gerald Barasa pamoja na afisa wa upelelezi wa jinai eneo la  Magarini Boaz Obeto, wamefika katika hospitali ya Malindi na kusema kuwa wameidhinisha uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Tayari wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu kutoka Magarini wakiongozwa na Pola Kenga wa shirika la Sauti ya wanawake wamehimiza uchunguzi kufanywa mara moja na wahusika kuadhibiwa kisheria.

Taarifa na Charo Banda.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.