Msambweni Chapter waibuka mabingwa

June 25, 2018

Timu ya wachezaji wa soka wasiozidi umri wa miaka 12 kutoka Msabweni ndio mabingwa wa makala ya tano ya Samba Sports yaliyoandaliwa katika uwanja wa maonyesho wa Diani.


Msambweni walinyakua ubngwa kwa kuwalaza King Boys mabao 2-1 katika fainali.

King Boys walifika fainali kwa kuwalaza Kombani Chapter bao 1-0. Nao Kombani waliwaangusha Kwale Chapter 1-0.

Katika mechi za awali, Kwale Chapter walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Schalke 04 FC. Green Marines wakatoka sare ya 1-1 na Msambweni katika muda wa kawaida. Kupitia kwa michuti ya penanti Msambweni walifunga penanti 5 nao Green Marines wakapa 4.

Kombani Chapter waliandikisha ushindi wa 2-0 dhidi ya Amsterdam FC.
King Boys FC wakatoka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Scheme FC.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.