Msanii awafokea walemavu bandia

May 20, 2018

Msanii wa mziki wa Bango kwa jina Duncan Mole kutoka kwa kundi la Afro Tambo amewafokea walemavu bandia.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Mole ameitaja hatua ya watu wasiokuwa na kasoro ya mwili kuomba omba barabrani kama isiyofaa na inayopaswa kusitishwa.

Mwanamziki huyo ambaye kupitia usemi huo amethibitisha kuwa ni mlemavu, amewahimiza watu kutia bidii badala ya kubakia omba omba barabarani.

“BEGGERS BEGGERS BEGGERS: usijifanye mlemavu kusudi watu wakuhurumie na ufaidike kwa kisingizio cha huna uwezo. Sisi wenyewe tu walemavu na hatuendi huko barabarani kuomba, mbona wee uende? Kila kaunti ingetoa hao BEGGERS kwa streets. Kila mtu ale jacho lake.sorry to say this but vimniesinya kufikia hapo,” aliandika Mole.

Duncan Mole ni mmoja kati ya wasanii wanaofanya vyema kwenye mziki wa Bango ukanda wa Pwani. Anasifika kwa vibao kama vile John na Doreen maarufu kama Zizimo na Maluani, na Mapenzi ni Basi.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.