MSICHANA (19) AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMNAJISI MVULANA (17)

December 4, 2017

Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 19 amefikishwa katika mahakama ya mjini Kwale kwa kosa la kumnajisi mtoto wa kivulana mwenye umri wa miaka 17.

Kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya Kwale Timothy Musyoki ameiambia mahakama kwamba kati ya tarehe 1 na3 mwezi Disemba mwaka huu, Mwanalima Nassoro alisababisha uke wake kuingiliwa na uume wa mtoto husika katika eneo la Tukutane Ukunda kaunti ya Kwale.

Akiwa mbele ya hakimu Doreen Mulekyo, Mwanalima Nassoro amekanusha shtaka hilo.

Kesi hiyo itaskizwa tena tarehe 14 mwezi Disemba mwaka huu.

Taarifa na Mimu Mohammed

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.