Mteza watwaa ubingwa Kwale

July 7, 2018

MTG

Timu ya wasichana ya Mteza ndio mabingwa wa maka huu ya mashindano ya soka ya wanawake yanayoandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Moving the Goal Post.

Mteza wamepata ubingwa kwa kuwabwaga Mwangaza kwa mabao 3-0.

Jumla ya timu tano zilishiriki katika mashindano hayo. Timu hizo ni Jorori, Mteza, Kenya Calcium, Kombani na Mwangaza.

Mchuano huo umefanyika katika shule ya msingi ya Kwale.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.