Mtoto ambaye babake alikanyagwa na ndovu ashindwa kujiunga na shule ya upili

January 13, 2018

Ndoto ya kuwa daktari kwa mwanafunzi mmoja mwenye umri wa miaka 15 kutoka mtaa wa Kinarini mjini Kwale, huenda ikakosa kutimia baada ya mwanafunzi huyo kukosa karo.

Said Mwarahani aliyefanya mtihani wa KCPE katika shule ya msingi ya Ziwani gatuzi dogo la Matuga, na kupata alama 323 na kuitwa katika shule ya upili ya Mazeras, ameshindwa kujiunga na kidato cha kwanza, akidai kuwa mamake ameshindwa kugharamia karo.

Mwanafunzi huyo aliye na ndoto ya kuwa daktari katika siku za usoni, alitarajiwa kuripoti shuleni siku ya Jumanne juma hili, sasa anawaomba wasamaria wema  kumsaidia kugharamia karo ya shule.

Mamake mwanafunzi huyo, amesema kuwa mumewe alifariki baada ya kukanyagwa na ndovu, huku akielezea hali ngumu anayopitia kuwalea watoto wake 7 walioachwa nyuma.

Taarifa na Michael Otieno.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.