Mtoto wa umri wa miaka 14 ajinyonga

May 30, 2018

OCPD GERALD BARASA 2

Afisa mkuu wa Polisi eneo la Magarini kaunti ya Kilfi Gerald Barasa, amesema Polisi wameanzisha uchunguzi kuhusiana na tukio la mtoto wa umri wa miaka 14 kujitoa uhai katika kijiji cha Boyani.

Barasa, amesema Marehemu Charles Kadenge aliye mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi ya Boyani, akiwa na wenzake waliiba kipatakilishi kwenye shule hiyo na kutoweka na kisha baadaye akapatikana akiwa amejitoa uhai.

Amesema huenda ikawa ndio chanzo cha mtoto huyo kujitoa uhai, japo amewataka Wazazi, walimu na jamii kuwachunguza vyema watoto wao na kuwapa ushauri nasaha badala ya kutoa vitisho vinavyopelekea kushuhudiwa kwa visa kama hivyo.
Kwa sasa mwili wa mwendazake unahifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali kuu ya Malindi kaunti ya Kilifi.

Taarifa na Esther Mwagandi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.