MUHURI yatamaushwa na kashfa za ufisadi nchini

May 30, 2018

Shirika la kutetea haki za kibinadamu nchini la MUHURI limeelezea kutamaushwa na kashfa nyingi za ufisadi zinazokumba taasisi nyingi za kiserikali nchini.

Kupitia kwa mkurugenzi wake Hassan Abdille shirika hilo limesema kwamba Uzembe wa viongozi walio mamlakani ndio chanzo kikuu cha kushuhudiwa kwa kashfa nyingi za ufisadi nchini.

Akizingumza na wanahabari katika afisi za shirika hilo mjini Mombasa Abdille amempongeza mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma nchini Nurdin Hajj kwa kuwakamata washukiwa wanaodaiwa kujihusisha na ufisadi kwenye sakata ya idara ya huduma ya vijana kwa taifa NYS.

Shirika hilo limetishia kuwashawishi wananchi kuandaa maandamano ya kitaifa ikiwa serikali haitalichukulia kwa uzito swala la ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma.

Kauli ya shirika hili inajiri huku washukiwa 33 kati ya zaidi ya 50 wanaohusishwa na sakata ya shilling bilioni 9 za shirika la huduma ya vijana kwa taifa NYS kufikishwa mahakamani jana.

Taarifa na Cyrus Ngonyo na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.