Mung’aro amtaka Rais Kenyatta kujitenga na viongozi wasio na ajenda za kimaendeleo

January 1, 2018

Aliyekuwa Mbunge wa Kilifi kaskazini Gedion Mung’aro amemtaka Rais Uhuru Kenyatta kushirikiana kikamilifi na viongozi wenye ajenda za kulinufaisha taifa na maendeleo na wala sio wenye malengo binafsi.

Mungaro amesema kwamba taifa hili linastahli kusonga mbele kimaendeleo na viongozi wanafaa kushirikiana kuliendeleza na wala sio kuendeleza malumbano yasiyokuwa na msingi.

Akizungumza mjini Mombasa Mung’aro amemshinikiza Rais Kenyatta kujiepusha na viongozi wasiokuwa na ajenda za maendeleo na kufanyakazi na viongozi ambao wako tayari kufanikisha ajenda za kimaendeleo za taifa.

Mbunge huyo wa zamani wa kilifi kazkazini aidha amewaomba viongozi wa upinzani kukomesha malumbano yao ya kisiasa na kushirikiana na serikali kuliendeleza taifa.

Taarifa na Cyrus Ngonyo.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.