Muungano wa shule za madereva waulaumu serikali

May 5, 2018

Taasisi zinazotoa mafunzo ya udereva nchini hazipaswi kulaumiwa na Serikali kwani zinajizatiti kuhakikisha kwamba madereva wanahitimu kabla ya kukabidhiwa leseni.

Naibu Mwenyekiti wa Muungano wa shule za udereva nchini John Magara amesema kwamba ni sharti taasisi hizo zitimize sheria hitajika na kutoa mafunzo ya hali ya juu kabla ya kumruhusu dereva kuanza kutoa huduma za uchukuzi barabarani.

Kulingana na Mwenyekiti huyo wa Muungano wa taasisi za mafunzo ya udereva hapa Pwani, ni lazima Wizara ya uchukuzi kuwahusisha kikamilifu wadau wote wa uchukuzi katika kujadili kuhusu jinsi ya kuimarisha hali ya usalama barabarani.

Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.