Mwadeghu awamwagia cheche wanasiasa wa Jubilee

May 8, 2018

05 07 17 MWANDEGU

Picha/ Maktaba

Mbunge wa zamani wa Wundanyi Thomas Mwadeghu, amewakosoa baadhi ya wanasiasa wa chama cha Jubilee wanaodai kuwa Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga anapanga kuwania kiti cha urais kwenye uchaguzi wa mwaka wa 2022.

Akongea mjini Naivasha katika kikao cha kamati kuu ya kitaifa ya chama cha ODM, Mwadeghu amesema kwamba lengo la Raila ni kuhakikisha kwamba wakenya   wanaishi kwa umoja, uiano na utangamano.

Mwadeghu  amewashauri viongozi wa vyama tanzu wa NASA,  Musalia Mudavadi, Kalonzo  Musyoka na Moses Wetang’ula,  kuweka tofauti zao za kisiasa kando na kuunga mkono juhudi za rais  Uhuru Kenyatta na Raila Odinga kuliunganisha taifa.

Juma lililopita baadhi ya wabunge wa chama cha Jubilee wanaoegemea upande wa Naibu rais William Ruto, walidadi kuwa Raila anapanga mikakati ya kuwania urais mwaka wa 2022.

Taarifa na Michael Otieno.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.