Mwenyekiti wa bodi ya Equity Group astaafu

June 7, 2018

Mwenyekiti wa Bodi ya Equity Group Holdings Dkt. Peter Kahara amestaafu na nafasi yake kuchukuliwa na David Ansell, aliyekuwa akihudumu kama Naibu Mwenyekiti wa kundi hilo.

Kahara ambaye amekuwa Mwenyekiti mwanzilishi tangu mwaka wa 1984, ameeleza tamanio lake la kustaafa kutoka kwa bodi hiyo ili kuadhimisha miaka yake ya 35 kwa bodi hiyo, akijitayarisha kuadhimisha mwaka wake wa 75 wa kuzaliwa.

Kahara na Ansell watafanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha mabadiliko hayo yanatekelezwa kwa utaratibu wakati wa mkutano wao mkuu wa kila mwaka utakaofanyika mwaka ujao.

Bodi hiyo imepongeza uongozi na hekima Kahara, uliochangia Benki ya Equity kutoka kiwango cha chini hadi sasa ikiwa ndiyo Benki kubwa zaidi inayotoa huduma za kifedha katika Bara la Afrika.

Taarifa na Michael Otieno.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.