Mwinyi awahimiza wazazi kuzingatia elimu

July 9, 2018

Wazazi katika eneo bunge la changamwe wamehimizwa kuzingatia zaidi elimu ya watoto kwa kuwekeza kwenye sekta hiyo.

Akiongea na wanahabari mjini Mombasa Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi amesema kuwa kwa muda mrefu viwango vya elimu vimeonekana kuwa duni na nisharti wazazi wazingatie elimu ya watoto wao ili kuimarisha viwnago vya elimu Pwani.

Mwinyi amesema kuwa kuna haja ya wazazi kushirikiana na wadau katika sekta ya elimu kama njia moja wapo ya kipiga jeki sekta hiyo.

Wakati uo huo amesema kuwa anamipango ya kuwekeza zaidi katika kuboresha miundo msingi katika shule za eneo hilo la changamwe mwaka jao wa kifedha.

Taarifa na Cyrus Ngonyo.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.