MZEE AULIWA BAADA YA MAZISHI JARIBUNI-KILIFI

June 14, 2018

Familia moja ya zaidi ya watu 20 katika kijiji cha Mayowe eneo la Jaribuni kaunti ya Kilifi, inaishi kwa hofu baada ya kundi la watu wasiojulikana kuvamia boma lao na kumuua mzee wa miaka 70.

Janet Chivatsi mtoto wa mwendazake Chivatsi Mzungu amesema kisa hicho kilitokea baada ya mama mmoja mwengine kuvamiwa na kuuwawa na watu wasiojulikana.

Bi. Chivatsi ameeleza kuwa baada ya mazishi ya mama huyo, umati wote ulivamia boma lao na kumpiga mzee huyo kwa mawe kabla ya kumteketeza pamoja na mali zake zote.

Jackson Chivatsi mwanawe mwendazake, alipata uvumi kabla ya mazishi ya mama huyo kuwa familia yao ingevamiwa lakini hata baada ya kuwasilisha ripoti kwa idara husika, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.

Bw. Chivatsi amesema kwa sasa ndugu zake wawili wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Ganze katika kaunti ya Kilifi baada ya kuandikisha taarifa ya kifo cha baba yao.

Kwa upande wake Patrick Ngeiywa, afisa mkuu wa polisi eneo la Ganze, amesema vijana hao wanaozuiliwa ni washukiwa wa mauaji ya mama wa huku polisi wakiendeleza uchunguzi kuhusiana na kisa hicho.

Taarifa na Marieta Anzazi:

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.